Mbunge wa EALA Dkt. Shogo Mlozi afariki dunia

 

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, amelitangazia bunge taarifa za kutokea kifo cha Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) Dkt. Shogo Richard Mlozi.

Spika Tulia ametangaza kifo hicho leo Alhamisi June 13, 2024 kabla ya kuanza kwa kikao cha 46 cha mkutano wa 15 wa Bunge la 12 Bungeni Jijini Dodoma ambapo amesema taarifa zaidi zitatolewa baadaye.

“Leo asubuhi tumepokea taarifa kwamba Mh. Dkt. Shogo Richard Mloz ambaye tulimchagua kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki hatunae tena, hii ni taarifa ya awali tutakapopata taarifa za ziada tutawataarifu tusimame kwa dakika moja tumpe heshima zake za mwisho,” aliema Spika Dkt. Tulia.

Chapisha Maoni

0 Maoni