Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto
Biteko amekutana na kufanya mazungumzo na wawekezaji wa Modern Industrial Park
wanaomiliki kongani ya viwanda eneo la Kibaha, Mkoani Pwani.
Mazungumzo hayo yamefanyika jana katika ofisi za Naibu
Waziri Mkuu Bungeni, jijini Dodoma.
Aidha, Dkt. Biteko amewaeleza wawekezaji hao kuwa Serikali
iko tayari kushirikiana nao na kuwapatia umeme kwa ajili ya kuwezesha shughuli
za uwekezaji katika eneo hilo.
Naye, Mwakilishi wa kampuni ya Modern Industrial Park, Bw. Yusuf Manzi alisema kuwa eneo hilo lina uwezo wa kubeba viwanda 202 vya aina mbalimbali na tayari miundombinu wezeshi kama maji, Ulinzi na usalama pamoja na barabara vimeshawekwa kwa ajili ya kurahisisha uwekezaji katika eneo hilo ambalo lina uhitaji wa 200MW za umeme kwa ajili ya kutumika na wawekezaji.
Habari pamoja na picha zote na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati
0 Maoni