Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj
Dk.Hussein Ali Mwinyi amewaomba Waumini wa Dini ya Kiislamu kuendelea kuwaombea
Dua Viongozi ili watimize majukumu yao na kutekeleza ahadi walizoahidi.
Rais Dk. Mwinyi amesema hayo alipojumuika na Waumini wa Dini
ya Kiislamu katika sala ya Ijumaa Msikiti wa Qubaa Mbweni Mkoa wa Mjini
Magharibi tarehe 10 Mei 2024.
Pia Rais Dk. Mwinyi amewatembelea Wazee akiwemo Mbunge wa zamani Jimbo la Amani , Mzee Hassan Rajab nyumbani kwake Kisauni na Mjumbe wa Baraza la Wazee CCM Kisiwandui, Bi Maryam Hengwa nyumbani kwake kwa Mchina Mkoa wa Mjini Magharibi.
0 Maoni