Rais Samia aing’arisha Tanzania kwa Uhuru wa Habari

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amesaidia kwa kiasi kikubwa Tanzania kuongoza katika nchi za Afrika Mashariki kwa kuwa kinara wa kuheshimu uhuru wa habari kwa mwaka 2024.

Tangu aingie madarakani, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa ni muumini mkubwa wa uhuru wa habari, jambo ambalo limeifanya Tanzania kupanda kwa kasi katika viwango vya uhuru wa habari duniani.

Takwimu za World Press Freedom Index 2024, zimeonyesha Tanzania kufanya vizuri kwenye kuheshimu uhuru wa habari kwa kushika nafasi ya 97 kwa Mwaka 2024 toka nafasi ya 143 kwa Mwaka 2023.

Hii inamaana Tanzania imepanda kwa kasi kwa nafasi 46 na kuziacha nchi nyingine za ukanda wa Afrika ya Mashariki nyuma, ambapo Kenya imeshika nafasi 102, Uganda nafasi 128, DRC  nafasi 123, Rwanda nafasi 144, Sudan Kusini nafasi 136 na Ethiopia nafasi 141.

Hayo yanajitokeza ikiwa leo ni Mei 03, 2024 ambapo ni kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani.

Tanzania leo inaadhimisha maazimisho ya 31 ya siku hii tangu azimio la Windhoek nchini Namibia, ambapo kwa mwaka huu maadhimisho hayo yanafanyika Jiji la Dodoma, yakiwa na Kauli mbiu ya “Tuilinde Dunia kupitia uhuru wa habari”.

Chapisha Maoni

0 Maoni