Muhimbili yapokea msaada wa mashine yenye thamani ya TShs 16.9 mil

 

Hospitali ya Taifa Muhimbili imepokea msaada wa mashine POCUS yenye thamani ya TZS. 16.9 MIL kutoka kwa wafadhili wa mradi wa Himofilia (Novo Nordisk Foundation na Novo Nordisk Haemophilia Foundation) ambayo itahudumia wagonjwa wenye magonjwa ya damu (HIMOFILIA).

Akipokea msaada huo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji, Mkurugenzi wa Huduma za Tiba MNH, Dkt. John Rwegasha amesema mashine hiyo itatumika katika kufanya uchunguzi na kufuatilia maendeleo ya ugonjwa katika maungio ya wagonjwa na kusaidia kupunguza matumizi ya dawa yasiyokuwa ya lazima kwa wagonjwa wa Himofilia kwakuwa sio kila maumivu aliyonayo mgonjwa yanayosababisha na kuvuja damu.

Ameongeza kuwa mashine hiyo itawezesha mtalam kuona kama mgonjwa amevuja damu sehemu za ndani mathalani kwenye goti, tumboni au misuli kwa urahisi na haraka ambapo ingekuwa ngumu kutambua kwa macho. 

Ameongeza kuwa pamoja na kutoa msaada wafadhili hao pia wataendesha mafunzo ya siku nne ambapo yataanza tarehe 28 hadi 31 Mei, 2024 ambapo yatatolewa kwa wataalam wa Utengamao.

 “Ninawashukuru Wafadhili wetu Novo Nordisk Foundation na Novo Nordisk Haemophilia Foundation kwa uwezeshaji wao kwani pamoja na kutupatia msaada pia wametuletea mtaalam aliyebobea zaidi katika mashine hiyo ya POCUS kutoka nchini Kenya ambaye atawejengea uwezo wataalam wetu namna nzuri ya kutumia mshine hiyo,” amesema Dkt. Rwegasha.

Chapisha Maoni

0 Maoni