Jafo atua Katavi Kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.Dkt. Selemani Jafo amewasili katika uwanja wa ndege wa Mpanda, mkoani Katavi, katika Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani.

Akiwa Mkoani Katavi Mhe. Dkt. Jafo atatembelea Wilaya ya Tanganyika ambapo atapokea taarifa ya biashara ya Kaboni kutoka katika Vijiji nane, atakagua birika la kunyweshea Mifugo , ujenzi wa Zahanati ya Kapanga , nyumba za Watumishi na kukagua vyumba vya madarasa vya Shule ya msingi Kapanga.

Aidha 29/5/2024 Mhe. Jafo atatembelea Halmashauri ya Mpimbwe ambapo atatembelea kijiji cha Ntibili, msitu wa Masatu. Akiwa Ntibili, Dkt. Jafo atakagua chanzo cha Maji na kupanda miti. Sambamba na hilo atakabishi hati miliki za ardhi za kimila kwa wananchi na Taasisi kwa niaba ya Halmashauri 7 zinazotekeleza mradi wa Urejeshwaji Endelevu  wa Mazingira na Hifadhi ya Bioanuai Tanzania (SLR). Mradi huu unasimamiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais ( Muungano na Mazingira).

Chapisha Maoni

0 Maoni