Goli la Aziz Ki lilikuwa goli halali- Rais wa CAF

 

Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Patrice Motsepe amekiri kuwa goli la Yanga lililokataliwa mwamuzi katika mchezo wa robo fainali dhidi ya Mamelod Sundowns nchini Afrika Kusini lilikuwa goli halali.

Rais Motsepe ameyasema hayo leo alipowasili visiwani Zanzibar katika Fainali za African Schools Football na kupokelewa na mwenyeji wake Rais wa Shirikisho la Soka nchini TFF Wallace Karia.

“Japo Rais wa CAF hatakiwi kutoa maoni yoyote kuhusu maamuzi ya mwamuzi lakini kwangu mimi nilivyorudia kuangalia lilikuwa ni goli halali,” amesema Motsepe.

Goli hilo lilifungwa na kiungo wa Yanga Stephen Aziz Ki ambapo mwamuzi alilikataa kwa kile alichoamini mpira haukuvuka mstari wa goli.

Chapisha Maoni

0 Maoni