Rais Samia afanya mazungumzo na mgeni wake Rais wa Somalia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amempokea  rasmi Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Somalia Mhe. Dkt. Hassan Sheikh Mohamud wakati alipowasili katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 27 Aprili 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama pamoja na Mgeni wake Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Somalia Mhe. Dkt. Hassan Sheikh Mohamud wakati Wimbo wa Taifa wa Tanzania ukiimbwa katika mapokezi kwenye viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 27 Aprili 2024.

Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Somalia Mhe. Dkt. Hassan Sheikh Mohamud akisaini kitabu cha wageni mbele ya mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 27 Aprili 2024.

Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Somalia Mhe. Dkt. Hassan Sheikh Mohamud akikagua gwaride  wakati wa mapokezi rasmi katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 27 Aprili 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Mgeni wake Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Somalia Mhe. Dkt. Hassan Sheikh Mohamud mara baada ya kukamilisha ziara yake ya Kiserikali nchini Tanzania, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 27 Aprili 2024.

Chapisha Maoni

0 Maoni