Mvua kubwa ikinyesha usiruhusu mtoto aende shule

 

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, amewataka wazazi na walezi kutowaruhusu watoto wao kwenda shule pindi mvua inapokuwa imenyesha kubwa.

Akizungumza jana, Prof. Mkenda amesema mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini ni vyema wazazi wakachukua tahadhari ili kuepusha kutokea majanga.

"Mzazi ukiona mvua ni kubwa usimruhusu mtoto wako aende shule, akikosa siku moja ama mbili si mbaya, tunazipongeza shule ambazo zimechukua hatua za kusitisha masomo kipindi hiki," amesema Prof. Mkenda.

Hatua hiyo ya Prof. Mkenda inatokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha na kusababisha uharibifu wa miundombinuna na barabara kupitika kwa shida pamoja na baadhi ya shule kuzingirwa na maji.

Chapisha Maoni

0 Maoni