Mke wa Rais wa Zanzibar, Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya
Wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) Mhe.Mama Mariam
Mwinyi ametoa wito kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu kuendelea
kutenda mema , kuombeana baada ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kuendelea kuwasaidia watu wenye mahitaji
maalumu.
Mama Mariam Mwinyi amesema hayo alipotoa zawadi za mkono wa
Eid alipotembelea vituo mbalimbali vya kuwalea Wazee na Watoto ikiwemo kituo
cha kulea Watoto ZASO Fuoni
Mambosasa, kituo cha Wazee Welezo ,
kituo cha Wazee Sebleni , kituo cha
Watoto SOS na kituo cha Watoto
Mazizini , Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe: 10 Aprili 2024.
Aidha, Mama Mariam Mwinyi amesema ni wajibu kuwalea,
kuwatembelea na kuwaenzi Wazee kufanya hivyo ni baraka kubwa sana.
Halikadhalika Mama Mariam Mwinyi ameeleza kuwa Serikali itaendelea kuwasaidia Wazee na kuwajali.
Mke wa Rais wa Zanzibar, Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) Mhe.Mama Mariam Mwinyi akifurahia jambo pamoja na mtoto aliyembeba.
0 Maoni