Balozi: Tupinge rushwa kwa vitendo

 

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dk Emmanuel Nchimbi , amewataka Watanzania wote kujituma na kufanya kazi kwa bidii  huku kutojihusisha na vitendo vya kutoa au kupokea rushwa.

"Endeleeni kuchapa kazi kwa bidii , kufanya kazi zitakazokuingiza kipato kihalali lakini jiepusheni na rushwa kwakuwa siku zote ndio adui wa haki, kuchapa kazi ni kuendelea kuunga mkono juhudi za Rais Samia za kuwataka Watanzania wote kufanya kazi na ndipo tutazidi kulijenga taifa letu na kuimarika kiuchumi"

Vilvile, Balozi Balozi Nchimbi amesema Jeshi la CCM (Viogozi wa kitaifa) wataendelea kuhakikisha wanaisimamia serikali ipasavyo katika kutimiza wajibu wao na kutekeleza ilnai ya uchaguzi ya mwaka 2020/2025.

Balozi Nchimbi ameyasema hayo wakati alipopokelewa na vongozi, wanachama, wapenzi, mashabiki na wadau mbalimbali wa maendeleo katika ofisi za CCM Mkoa wa Mbeya.

Chapisha Maoni

0 Maoni