Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Hungary, Mhe. Péter
Szijjártó, amewasili nchini Tanzania kwa ziara ya kikazi ya siku mbili tarehe
27 na 28 Machi 2024.
Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Mhe.
Szijjártó alipokelewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Said Shaib Mussa.
Wengine walioshiriki katika mapokezi hayo ni Mkurugenzi Idara
ya Ulaya na Amerika, Balozi Swahiba Mndeme, Mkurugenzi wa Kitengo cha
Mawasiliano ya Serikali, Balozi Mindi Kasiga; Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya
Ulaya na Amerika, Bw. Gerald Mbwafu pamoja na Afisa Ubalozi wa Tanzania nchini
Hungary mwenye makazi yake nchini Ujerumani, Bi. Angela Ngailo.
0 Maoni