Waziri Mkuu ahudhuria mkutano wa wadau wa elimu

 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipewa maelezo na Mratibu wa Shughuli za Vijana mkoa wa Dodoma Almas Daruwesh kuhusu majukumu mbalimbali yanayoratibiwa na Chama cha Skaut, wakati wa Mkutano wa wadau wa elimu mkoa wa Dodoma kwenye ukumbi wa Chuo cha Biblia Mkoani Dodoma Machi 25, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akioneshwa na Mwalimu Selina Kadewele wa Shule ya Msingi Songambele-Kongwa zana ya kufundishia (Mfano wa Komputa mpakato) wanafunzi wa awali wakati wa Mkutano wa wadau wa elimu mkoa wa Dodoma katika ukumbi wa Chuo cha Biblia Mkoani Dodoma Machi 25, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akioneshwa na Mwanafunzi wa Kidato cha Sita wa Shule ya wasichana ya Msalato, Rosemary Brighton namna wanavyofanya mafunzo kwa vitendo ya upasuaji, wakati wa Mkutano wa wadau wa elimu mkoa wa Dodoma kwenye ukumbi wa Chuo cha Biblia Mkoani Dodoma Machi 25, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokea tuzo, kutoka kwa watoto Shule ya Msingi Kizota, kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Samia Suhulu Hassan, ikiwa ni kumshukuru kwa jitihada anazofanya katika miundombinu ya elimu, kuimarisha taaluma na michezo, kwenye mkutano wa wadau wa Elimu uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Biblia Mkoani Dodoma Machi 25, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokea tuzo, kutoka kwa Dada Mkuu wa Msalato Girls, Sylvia Florence, inayotambua juhudi zake katika usimamizi na utekelezaji wa miradi ya elimu nchini, kwenye mkutano wa wadau wa Elimu uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Biblia Mkoani Dodoma Machi 25, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Chapisha Maoni

0 Maoni