Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb)
leo Machi 20, 2024 amekagua
mabanda ya Maonesho yatakayotumika katika Maadhimisho ya Siku ya Misitu Duniani
na Siku ya Upandaji Miti Kitaifa yanayotarajiwa kufanyika Machi 21 ambapo Mgeni
Rasmi katika Kilele hicho anatarajiwa kuwa
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip
Isdor Mpango.
Akitembelea mabanda yaliyopo kwenye Maonesho hayo, Mhe.
Kairuki ameipongeza Wizara pamoja na Wadau wa misitu waliojitokeza kwa ajili ya
kutoa elimu kuhusu majukumu yanayotekelezwa na taasisi zao ikiwemo elimu ya
uhifadhi pamoja na kuonesha bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na mazao ya
misitu.
Mhe.Kairuki ametumia
fursa hiyo kuwataka Wakazi wote wa Wilaya ya Same, Mkoani Kilimanjaro pamoja na Mikoa ya jirani kujitokeza kwa
wingi kutembelea maonesho hayo.
Amesema maonesho hayo ni
muhimu kwao kwani wataweza kujifunza masuala mbalimbali ikiwemo elimu ya
ufugaji nyuki kibiashara pamoja na kujua fursa mbalimbali zinazopatikana katika
mnyororo wa thamani ya mazao ya misitu.
Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Misitu Duniani na Siku ya
Upandaji miti Kitaifa hufanyika kila mwaka Machi 21ambapo kwa mwaka huu Tanzania inaadhimisha Kilele hicho kwa
kupanda miti pamoja na kutembelea
maonesho ya bidhaa mbalimbali zitokanazo na
misitu na nyuki.
0 Maoni