Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.
Hussein Ali Mwinyi amepokea salamu za pole kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa
Kampuni ya Wasafi Nasibu Abdul Juma almaarufu Diamond Platinumz na ujumbe wake
Ikulu Mnazi Mmoja tarehe 20 Machi 2024.
Aidha Rais Dk. Mwinyi ameushukuru uongozi wa Wasafi kwa kuja
kumfariji na kushiriki katika mazishi ya Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi pamoja
na utayari wao kushiriki kutangaza mazuri yanayofanywa na Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar.
Halikadhalika Mkurugenzi Mkuu wa Wasafi Nassib Abdul
amempongeza Rais Dk. Mwinyi kwa kazi nzuri anayoifanya ya kuwaletea maendeleo
Wazanzibari na kuvuka malengo ya ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025 hususani
katika sekta ya elimu.
Vilevile Wasafi wameahidi kuendelea kushirikiana na Rais Dk. Mwinyi
na kumuunga mkono kuyatangaza mazuri yote anayotekeleza kwa wananchi wa
Zanzibar, pia wamemkabidhi zawadi ya nyimbo maalum kwa ajili ya kazi nzuri
alizofanya iliyotungwa na wasanii kutoka Wasafi.


0 Maoni