Jafo azindua vituo vitatu vya mradi wa EBARR

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Selemani Jafo (kulia) akishona nguo kwenye moja ya cherehani alizokabidhi wakati wa uzinduzi wa majengo ya Vituo vitatu (3) vya ujasiliamali wa ushonaji, na kukabidhi Vyerehani 21 na vifaa vingine vya ushonaji. Jumla ya Wajasiliamali 45 watanufaika na mradi huo wenye thamani ya shilingi milioni 43, kupitia mradi ulioratibiwa na EBARR.

EBARR ni Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia Ikolojia vijijini. Mradi huu unasimamiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais , ukiwa na lengo la kuwawezesha wananchi kuhimili mabadiliko ya tabianchi pamoja na shughuli mbadala za kuwaongezea kipato.

Uzinduzi na Makabidhiano hayo yamefanyika katika vijiji cha Kiegea, Kazania na Mbugani Wilayani Mpwapwa, Machi 19,2024.



Chapisha Maoni

0 Maoni