Serikali wilayani Nyamagana Jijini Mwanza imewaonya
wafanyabiashara wa sukari watakaojaribu kukiuka bei elekezi kutoka bodi ya
sukari iliyotolewa kwenye tangazo la serikali inayoelekeza mfuko wa kilo
hamsini wa bidhaa hiyo uuzwe laki moja na elfu arobaini huku kilo moja ikiuzwa
kwa shilingi elfu mbili mia nane hadi elfu tatu
Agizo hili limetolewa leo tarehe 8/3/2024 na Mkuu wa wilaya
ya Nyamagana Amina Makilagi wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini
kwake.
Aidha, Makilagi amewataka pia watendaji wa serikali kusimamia
kikamilifu bei ya bidhaa hiyo ili wananchi waipate kikamilifu.


0 Maoni