Waandishi wa habari wafariki dunia kwa ajali

 

Waandishi wa habari wawili wa mkoa wa Lindi wamefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea katika eneo la Nyamwage mkoani Pwani.

Wanahabari hao walikuwa wanatokea Jjini Dar es Saalam kurudi mkoani Lindi ambapo walipata ajali mnamo majira ya saa saba usiku wa kuamkia leo.

Waliofariki ni mwandishi wa habari wa Kampuni ya Sahara Media group Mkoa wa Lindi Josephine Kiberity pamoja na mwandishi wa habari wa Channel Ten mkoani Lindi Abdallah Nanda.

Chapisha Maoni

0 Maoni