Msemaji Mkuu wa Serikali atembelea TANAPA

 

Mkurugenzi wa idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bw. Mobhare Matinyi ametembelea Makao Makuu ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na kukutana na  Kamishna wa Uhifadhi wa TANAPA, Mussa Juma Kuji, na kisha kufanya kikao kifupi na Menejimenti ya TANAPA jijini, Arusha.

Bw. Mobhare Matinyi atafanya Ziara ya siku 3 kutembelea Hifadhi za Taifa kuanzia Jana tarehe jana Machi 5 2024 na kujionea shughuli za Utalii na Uhifadhi na kukagua miundombinu hasa barabara katika Hifadhi ya Taifa Serengeti.



Chapisha Maoni

0 Maoni