Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini
(TARURA) Mhandisi Victor H. Seff ameongoza Kamati ya Utendaji ya Mradi wa RISE
Machi 14, 2024 kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara za Wenda-Mgama (19km) na
Mtili-Ifwagi-Mkuta (14km) kwa kiwango cha lami.
Ujenzi huo unatekelezwa na Mkandarasi CHICO katika
Halmashauri za Wilaya ya Iringa na Mufindi.
Msimamizi Mshauri wa Mkandarasi Afrisa ameeleza maendeleo ya
mradi yapo chini kutokana Mkandarasi kutokukamilisha idadi ya Mitambo na
Watumishi katika eneo la Kazi.
Hata hivyo, Mkandarasi CHICO ameahidi kumaliza kazi kwa muda
uliowekwa kwenye mkataba.
Mhandisi Seff amemtaka Mkandarasi CHICO kuongeza kasi ya
ujenzi ili kufidia muda uliopotea na ifikapo mwezi juni mwaka 2024 kama
atashindwa kufikia malengo yaliyowekwa kwa mujibu wa mkataba hatasita kuvunja Mkataba.
Miradi yote miwili inatarajiwa kukamilika hadi kufikia mwezi
februari, 2025.
Mradi wa RISE unalenga kuboresha barabara zenye fursa za
kiuchumi hasa maeneo yenye uzalishaji wa mazao ya kilimo kwa kujenga barabara
za lami.
Pia, kufanya matengenezo na kuboresha maeneo Korofi (bottleneck) ya mtandao wa
barabara za Wilaya ili kukuza uchumi na kuongeza fursa za ajira.
Mradi wa RISE unatekelezwa na TARURA kwa kipindi cha miaka
sita kuanzia mwaka wa fedha 2021/2022 hadi 2026/2027.
0 Maoni