Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akizungumza na wageni wake Rais Yoweri Museveni wa Uganda na Rais
William Ruto wa Kenya walipowasili Ikulu ndogo Tunguu Zanzibar jana tarehe 14 Machi,
2024.
Kwenye mazungumzo yao wamezungumzia masuala ya mtangamano wa
Afrika Mashariki hususan umuhimu wa kuharakisha zoezi la kukusanya maoni ya wananchi
Juu ya muundo na maeneo ya kuangaliwa katika Rasimu ya Katiba ya Fungamano la
kisiasa la Afrika Mashariki (EAC Political Confederation).
Zoezi hilo limeshafanyika katika nchi za Burundi, Uganda na
Kenya na linatekelezwa na timu ya wataalamu inayoundwa na wajumbe watatu kutoka
kila nchi mwanachama.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan, Rais Yoweri Museveni wa Uganda na Rais William Ruto wa Kenya
wakiangalia picha ya Viongozi wa Nchi mbalimbali za Afrika wakati Rais Museveni
alipomkabidhi Rais Samia zawadi hiyo baada ya mazungumzo yao Ikulu ndogo Tunguu
Zanzibar jana tarehe 14 Machi, 2024.
0 Maoni