Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii imeitaka mipango ya matumizi ya ardhi inayotekelezwa katika vijiji mbalimbali nchini kusimamiwa ipasavgo na Kamati za Vijiji ili iweze kuleta tija katika vijiji husika.
Aidha, Kamati hiyo ya Kudumu ya Bunge imeipongeza Wizara ya
Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Tume ya Taifa ya Matumizi ya Ardhi kwa
kazi nzuri inayoifanya kutekeleza miradi ya mipango ya matumizi ya ardhi kupitia
Tume ya Taifa ya Matumizi ya Ardhi katika vijiji mbalimbali nchini.
Kwa mwaka 2023/2024 wizara ya ardhi kupitia Tume ya Taifa ya Matumizi ya Ardhi na wadau wengine
imewtekeleza miradi ya mipango ya matumizi ya ardhi katika vijiji 333 kwa nchi nzima.
Mradi wa upangaji matumizi ya ardhi unatekelezwa na Wizara ya
Ardhi kupitia Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi ambayo imepewa
jukumu kubwa kisheria la kuwezesha na kuandaa mipango ya matumizi ya ardhi
katika ngazi mbalimbali nchini. Mipango hiyo huandaliwa katika ngazi ya Taifa,
Kanda, Mikoa, wilaya na vijiji.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na
Utalii Mhe, Timotheo Mzava akiwa katika ziara ya Kamati yake tarehe 13 Machi
2024 katika kijiji cha Namkatila halmashauri ya wilaya ya Ruangwa mkoa wa Lindi
amesema, kupanga mipango ya Matumizi ya ardhi ni jambo moja na kuisimamia na
kutekeleza ni jambo lingine.
Amebainisha kuwa, kazi ya kusimamia mipango ya matumizi ya
ardhi katika vijiji siyo ya waziri, Tume na wala wakuu wa wilaya na ndiyo maana zipo kamati za vijiji
zilizotokana na wananchi wa vijiji husika.
"Niombe mipango ya matumizi ya ardhi iliyotumia fedha za nchi na walipa kodi
kuitengeneza ikasimamiwe na kuheshikiwa na wenzetu katika kamati wasaidie ili
mipango hiyo ikalete matokeo na matumda
yaliyokusidiwa". Alisema Mhe, Mzava.
Tukiwa na mipango tunajisifia tumeipanga halafu hatuifuati
itakuwa ni kazi ya bure na huko vijjjini wenyevi na wenzake wakuendelea na
ujanja ujanja wa kuuza maeneo bila kufuata mipango iliyopangwa hatuwezi kutoka
na haiwezi kutusaidia" alisema Mhe, Mzava
Awali Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Mhe, Geophrey Pinda amesema, utekelezaji wa miradi ya upangaji matumizi bora ya
ardhi katika vijiji mbalimbali nchi ni juhudi za wizara yake kuona vijiji vyote
vinakuwa katika mpangilio mzuri.
Amesema, kwa wilaya ya Ruangwa Tume ya Taifa ya Matumizi ya
Ardhi imeweza kutekeleza mradi katika vijiji 16 na kutaja baadhi ya vijiji
hivyo kuwa ni Chikwale, Chihundu, Nambilanje, Mkaranga, Nanganga, Chikoko na
Likwachi.
Kwa mujibu wa Mhe, Pinda, Tume imewezesha uandaaji mipango
kina wa maeneo ya makazi kwenye kijji cha Namkatila uliowezesha uandaaji wa
hati za kimila 787 na upimaji mipaka ya vijiji 10 pamoja na upimaji mIpaka ya
vijiji uliowezesha utatuzi wa migogoro ya mipaka ya muda mrefu hususan mgogoro
wa moaka kati ya vijiji vya Nanjaru na Mnyangala vilivhopo katika manispaa ya
Lindi.
Aidha, Mhe, Pinda ameishukuru Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Ardhi kwa utashi walionao na kueeleza kuwa, umetoa msukumo wa kuongeza kasi ga uandaaji mipango ya matumizi ya ardhi ya vijiji ambayo
ni nyenzo muhimu katika utatuzi na udhibiti wa migogoro ya matumizi ya ardhi
nchini inayoendelea kuwa kero kwa wananchi kwa muda mrefu
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii
imefanya ziara ya kukagua utekelezaji wa
mradi wa kupanga matumizi ya ardhi katika halmashauri ya wilaya ya Ruangwa .
Aidha, Kamati pia ilikabidhi vyeti vya ardhi ya vijiji, ramani za mipaka iliyopimwa
na kuhuishwa, mipango ya matumizi ya ardhi ya vijiji na Hati za Hatimiliki za
kimila kwa wanachi.
Na. Munir Shemweta- Ruangwa
0 Maoni