Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii
imeridhia Mpango na Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu na taasisi zilizopo chini ya ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/25.
Aidha, Kikao cha kamati hiyo kilichofanyika jana bungeni
jijini Dodoma kikiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. Fatuma Toufiq
ambapo ameipongeza Wizara hiyo kwa kuandaa bajeti ambayo itawezesha utekelezaji
wa majukumu sambamba na kuleta mageuzi katika sekta ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu.
Katika kikao hicho Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako ameongozana na Naibu Waziri wa ofisi yake Mhe. Patrobas Katambi pamoja na Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Mhe. Mhandisi Cyprian Luhemeja kuiongoza Menejimenti na Wakuu wa taasisi zilizopo chini ya ofisi hiyo kuwasilisha bajeti hiyo.


0 Maoni