Askari wa Jeshi la Uhifadhi (JU) nchini wametakiwa kuzingatia
uwadilifu na misingi ya Jeshi hilo ili malengo ya Wizara ya Maliasili na Utalii
kupitia Jeshi hilo yaweze kufikiwa na kwa askari yeyeto atakaekiuka taratibu, kanuni na sheria
hatua kali zitachukukiwa dhidi yake.
Wito huo umetolewa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili
na Utalii Kamishna Benedict Wakulyamba Wilayani Biharamuro Mkoani Kagera,
alipokuwa akizungumza na uongozi wa Hifadhi ya Taifa Chato, na askari wa Jeshi
la Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi ya Taifa Tanzania (TANAPA) na Wakala wa
Misitu Tanzania (TFS).
CP Wakulyamba licha ya kuwapongeza askari hao kwa kazi nzuri
wanazofanya, amesisitiza kuwa, uongozi wa Wizara hiyo hautoa mvumilia askari askari yeyote atakae kwamisha jitihada
za Wizara za usingizi bora wa Uhifadhi
hususani katika kupambana na ujangili, mifugo ndani ya Hifadhi na Uchomaji moto
Misitu iliyohifadhiwa kisheria.
Awali akitoa Taarifa za ya utekelezaji wa majukumu ya Hifadhi
ya Burigi Chato, Mkuu wa Hifadhi Burigi Chato, Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi
Ismail Omari Ismail, amesema ndani ya muda mfupi wa uongozi wake wamefaniliwa
kupamba na uingizaji wa mifugo ndani ya Hifadhi kwa asilimia 225 kutoka Januari
2022 - February 2023 mifugo 13,839 hadi
6, 154 kwa Januari 2023 - Februari 2024 na kuwa zoezi hili ni lakudumu.
Aidha, Ismail kwa niaba ya watumishi wengine ameahidi
kufanyia kazi maagizo yote waliopewa na uongozi wa Wizara hususani kusimamia
nidhani ya askari, kubuni njia mbalimbali za kiuchumi na kuimarisha mahusiano
mema, na viongozi wa Serikali ngazi ya Mkoa hadi Vijiji pamoja na wanchini
waishio pambezoni mwa Hifadhi.
Katika hatua nyingine CP Wakulyamba amekutana na Kamati ya
Ulinzi na usalama Wilaya ya Biharamuro
na kuupongeza uongozi wa Wilaya hiyo kwa ushirikiano unaotoa katika uhifadhi wa
Hifadhi ya Burigi Chato, na kuahidi kuwa Wizara ya Maliasili na Utalii chini ya
Waziri Mhe. Angellah Kairuki itaendelea kushirikiana vyema na uongozi wa Wilaya
hiyo.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Biharamuro SACP. Advera Bulimba
amesema, hapendezwi kuona baadhi ya watu
wanafanya shughuli za kijamii ndani ya Hifadhi kama vile kilimo, uchomaji wa
Mkaa na ufugaji hivyo Kamati ya Ulinzi
na Usalama chini yake itaendelea
kushirikiana na Wizara ili kutokomeza changamoto hiyo ili Hifadhi hiyo iendelee
kuwa neema kwa wanachi wa Biharamuro na Tanzania kwa ujumla.
0 Maoni