Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imetoa
mafunzo kwa waandishi wa Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira (JET)
kuhusu utoaji wa habari za utatuzi wa migongano baina ya Binadamu na wanyamapori huku ikiwataka
waandishi hao kuzingatia weledi katika
kuelimisha jamii hasa katika utoaji wa taarifa zinazohusiana na migongano baina ya Binadamu na Wanyamapori ili ziweze
kuwasaidia waandishi hao waweze kutoa
taarifa sahihi ambazo mwisho wa siku zitasaidia Taifa katika suala zima la uhifadhi.
Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 22 Februari, 2024 na Mkuu wa
Kitengo cha Mawailiano cha Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw. John Mapepele
alipokuwa akifungua Mafunzo ya siku mbili ya waandishi wa habari
yaliyoaandaliwa na GIZ kupitia Mradi wa kutatua changamoto ya migongano baina
ya binadamu na wanyamapori katika Ukanda wa Ruvuma Mkoa wa Lindi katika Wilaya
ya Liwale na Ruvuma, Wilaya za Namtumbo na Tunduru kwa kushirikiana na
Serikali, yaliyofunguliwa leo Bagamoyo mkoa wa Pwani.
Mapepele amesema kwa sasa wizara ina falsafa mbili
kubwa ambazo ni uhifadhi na Utangazaji utalii na hivyo mafunzo hayo lengo lake kuu ni
kusaidia katika kuimarisha uhifadhi ili
usaidie katika utangazaji Utalii suala mabalo ni muhimu kwa jamii na Taifa kwa
ujumla.
"Uhifadhi ukiimarika mazao ya uhifadhi pia yataimarika
kama vile utalii na hivyo kulifanya taifa kupata fedha za kigeni na kuimarisha
uchumi wake kupitia hifadhi zetu," alisema
Mapepele.
Ameongeza kuwa, Wizara imewekeza nguvu kubwa katika njia
bora na za kisasa kutangaza Utalii na kuhifadhi huku akimpongeza Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea
kuimarisha uhifadhi ambapo amehakikisha uhifadhi unaendelezwa kwa ajili ya
Vizazi vya sasa na vizazi vya baadae.
Aidha, Mapepele amewataka wanahabari hao kutumia siku hizo
mbili za mafunzo ambazo zitawasaidia wanahabari hao kujengewa uwezo kwa ajili
ya kutoa habari za rasilimali zetu kwa faida ya Taifa kwa ujumla
“Niseme tu kwamba ni vizuri sana katika kipindi hiki sasa
mbapo tutakuwa hapa kwa siku mbili tutumie fursa hii adhimu vizuri kwani
itatusaidia sana kutujengea uwezo kwasababu katika nchi nyingi ambazo
zimeendele hufanya haya tunayofanya leo,’’ alisema Mapepele.
Ameongeza kuwa nchi ya Tanzania ni moja ya nchi ambayo
imepiga hatua kubwa katika eneo la uhifadhi ambapo asilimia 32 ya nchi
imehifadhia jambo ambalo ni la kupongezwa.
Naye Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira (JET), John Chikomo ameishukuru GIZ pamoja na Serikali kwa kuandaa mafunzo hayo ambayo kiujumla yatawasaidia waandishi hao kutoa Habari za migongano baina ya binadamu na wanyamapori kwa ufasaha na weledi mkubwa.
0 Maoni