Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.
Hussein Ali Mwinyi amekutana na Balozi wa Canada nchini Tanzania, Kyle Nunas na
ujumbe wa Wenyeviti wa Jumuiya ya Mabunge ya Canada na Afrika wakiongozwa na
Seneta, Amina Gerba Ikulu Zanzibar tarehe:22 Februari 2024.
Rais Dk. Mwinyi amesema sekta kuu ya uchumi wa Zanzibar ni
utalii ambao unachangia asilimia 30 ya pato la Taifa, pia ameikaribisha Canada
kuangalia fursa zilizopo katika uchumi
wa buluu ikiwemo utalii, uvuvi, usafiri wa vyombo vya baharini, bandari ,
mafuta na gesi.
Halikadhalika Rais Dk. Mwinyi ameishukuru Serikali ya Canada
kwa ushirikiano wa miradi mbalimbali ya huduma za kijamii ikiwemo elimu na
afya.
Vilevile Rais Dk. Mwinyi amesema Muungano wa Tanzania ni wa
kipekee utaendelea kuwa mfano wa kuigwa Afrika.
Pia katika mazungumzo hayo amegusia suala la uhuru wa habari, Serikali ya umoja wa kitaifa, nafasi za uwakilishi kwa Wanawake, uwekezaji pamoja na nishati hususani umeme.
0 Maoni