Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango amesema mfumuko wa bei
nchini umeendelea kudhibitiwa ambapo kwa kipindi cha Julai hadi Desemba mwaka
2023 ulifikia wastani wa asilimia 3.2, kiwango ambacho kipo ndani ya lengo la
kati ya asilimia 3 hadi asilimia 7.
Akizungumza katika Jukwaa la Kodi na Uwekezaji jijini Dar es
Salaam, Dkt. Mpango amebainisha kuwa katika mwaka 2023 pato la Taifa
limekadiriwa kukua kwa asilimia 5.0 ikilinganishwa na asilimia 4.7 mwaka 2022
na kwamba matarajio kwa mwaka 2024 ni kufika asilimia 5.5.
Aidha, ameongeza kuwa Tanzania imeendelea kuwa kitovu cha uwekezaji na nchi yenye uchumi unaokua kwa kasi Kusini mwa Jangwa la Sahara, licha ya misukosuko ya kiuchumi na kijamii inayoendelea duniani kote.
0 Maoni