Mkazi wa Ngara mkoani Kagera Bw. Charles Mwakameta amepungua
kilo 58 baada ya kuwekewa puto maalum (intragastric ballon) katika Hospitali ya
Taifa Muhimbili Mloganzila na kukaa na puto hilo kwa takribani mwaka mmoja.
Bw. Mwakameta amepunguza uzito kutoka kilo 151 alizokuwanazo
kabla ya Februari 20, 2023 alipowekewa putohadi kufikia kilo 92.65 alipotolewa
puto hilo Februari 26, 2024.
Akielezea kuhusu safari yake ya kupungua uzito Bw. Mwakameta
amesema ilianza baada ya kumuona msanii @peter_msechu ambaye aliwekewa puto
hospitalini hapa na kuona kwamba huduma hii ni ya kweli na ina matokeo mazuri.
“Kipindi nilipokuja kuwekewa puto nilikuwa na kilo 151
lakini mpaka leo nimekuja kutoa puto baada ya mwaka mmoja nina kilo 92.65, watu
walikua wakinicheka kutokana na uzito uliokithiri pia ninataka kuwaasa
watanzania wenzangu wenye matatizo ya uzito mkubwa kuweka puto kunasaidia
kupunguza uzito na wasiogope,’’ameeleza Bw. Mwakameta.
Kufuatia matokeo hayo mazuri ameishauri kufika katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila ili kupata huduma ya kuweka puto ambayo
imemsaidia na hajapata madhara yoyote zaidi ameweza kubalilisha mfumo wake wa
maisha.
Muhimbili Mloganzila ilianzisha huduma ya kupunguza uzito kwa kutumia puto (intragastric balloon) ambapo tangu kuanzishwa kwa huduma hii Novemba 2022 takribani wananchi 158 wamenufaika na huduma hiyo.
0 Maoni