MOI kuandaa kongamano kujadili ajali za bodaboda

 

Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) inatatarajia kuandaa kongamano kubwa la kitaifa la kutathimini na kujalidi hali ya usalama barabrani kutokana ongezeko la ajali hasa za bodaboda ili kuibua mbinu mpya za kukabiliana na janga hilo

Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Prof. Abel Makubi amebainisha hayo leo Februari 26, 2024 katika mahojiano ya mbashara ya kipindi cha Kumepambazuka kinachorushwa na Redio One.

Prof. Makubi amesema kongamano hilo linatarajia kufanyika Mwezi wa Tano mwaka huu na kwamba wadau wote wa sekta ya usafirishaji watahusishwa ili kupata mawazo chanya ya kukabiliana na ajali za barabarani hususani bodaboda.

“Katika kitengo chetu cha dharura asilimia 60 ya wangonjwa wanapokelewa pale ni wa ajali, kati ya hao asilimia 35 hadi 40 ni ajali za bodaboda, wengi wa hawa ni wanaume...vijana ambao ni nguvu kazi ya Taifa,” amesema Prof. Makubi na kuongeza.

“Tunatarajia kufanya kongamano litakalohusisha wizara ya afya na wadau wengine wote kwa usafiri wa barabara ili tutathimini wapi hapako sawa, kama kila mtu anatekeleza waji bu wake vipi mbona ajali zinaongezeka?”

Mkurugenzi huyo ametoa wito kwa bodaboda kujiunga na mfuko wa bima ya afya ili waweze kutibiwa kwa urahisi wanapopata ajali au maradhi mengine.

“Nina amini bodaboda wanaweza kujiunga na bima ya afya kwa kutoa kiasi kidogo katika kile wanachopata, kama bodaboda anaweza kupata 10,000 kwa siku nadhani anaweza kujiunga na bima ya afya,” amesisitiza.

Na Abdallah Nassoro- MOI

Chapisha Maoni

0 Maoni