IGP aagizwa kupeleka Polisi Kata maeneo yote nchini

 

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Jumanne Sagini amemuelekeza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Camilius Wambura kuhakikisha maeneo yote nchini yanapatiwa Wakaguzi Kata (Polisi Kata).

Amesema polisi hao wapelekwe katika maeneo ambayo bado hawajapelekwa askari hao kwa kuwa ajira zilizotolewa zinatosha kuwezesha kata zote kupata Askari kwa kiwango cha Mkaguzi wa Kata.

Sagini ameyasema hayo alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa jimbo la Mpwapwa, George Malima aliyeuliza kwa kuwa utaratibu wa kupeleka polisi jamii katika kata umeonesha mafanikio makubwa, ni lini Serikali itapeleka Polisi Jamii katika jimbo la Mpwapwa na kuwapatia pikipiki kwa wachache ili kurahisisha utekelezaji wa majukumu yao.

Aidha, Sagini amesisitiza kuwa ni maelekezo ya Serikali kuwapeleka Wakaguzi hao wa Kata kwenye Kata zote nchini ili kuhakikisha kata zote zinapata askari.

Chapisha Maoni

0 Maoni