Muhimbili na AFF wasaini mkataba wa kuboresha huduma za afya

 

Hospitali ya Taifa Muhimbili imesaini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano na Taasisi ya Africa Future Foundation (AFF) uliojikita katika maeneo mbalimbali ya kuwajengea uwezo wataalamu.

Akizungumza wakati wa kusaini mkataba, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Mohamed Janabi amesema Africa Future Foundation pamoja na Korea Foundation For International Health Care (KOFIH) wamekua wakishirikina na Muhimbili kwa muda mrefu ambapo wamekua wakitoa mchango mkubwa katika kuboresha utaoaji wa huduma za afya Muhimbili Mloganzila.

“Tunawashukuru sana kwa ushirikiano ambao umekuwa na manufaa makubwa kwa hospitali yetu ni matumaini yetu kwamba mkataba huu utaenda kuleta tija zaidi katika kuendelea kuboresha huduma za matibabu Muhimbili,”amesema Prof. Janabi.

Kwa upande wake Rais wa Taasisi ya Africa Furure Foundation Dkt. Soen Cheol Hong ameeleza kuwa mkataba huo utaenda kuwa na manufaa makubwa katika kuifanya Muhimbili Mloganzila  kuwa kituo cha umahiri katika tiba katika maeneo mbalimbali.

Maeneo hayo ni pamoja na kuwajengea  uwezo wataalamu katika kuimarisha huduma za matibabu ya figo, kutengeneza mishipa ya kudumu ya kuchujia damu kwa wagonjwa wenye changamoto ya figo, kuweka mpira wa kudumu wa kuchujia damu kifuani, kurekebisha na kuzibua mshipa wa kuchujia damu, kurekebisha na kuzibua mpira wa kuchujia damu.

Aidha, maeneo mengine ni huduma za magonjwa ya dharura, huduma ya mama na mtoto, huduma za uuguzi pamoja na vifaa tiba.

Chapisha Maoni

0 Maoni