Waziri Mkuu Majaliwa ahudhuria mkutano wa NAM

 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akishiriki ufunguzi wa mkutano wa 19 wa Wakuu wa Nchi na Serikali Zisizofungamana na Upande Wowote (NAM), katika ukumbi wa Ruwenzori, Kampala nchini Uganda, Januari 19, 2024. Waziri Mkuu amemuwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mkutano huo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Rais wa Jamhuri ya Cuba Miguel Mario Diaz-Canel Bermudez akimkabidhi rasmi Rais wa Uganda Yoweri Museveni uenyekiti wa kundi la Umoja wa Nchi na Serikali 120 zenye Msimamo wa Sera ya Kutofungamana na Upande Wowote (NAM) katika ukumbi wa Ruwenzori, Kampala nchini Uganda, Januari 19, 2024. Mheshimiwa Majaliwa amehudhuria mkutano huo kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Rais wa Uganda Yoweri Museveni, akizungumza baada ya kukabidhiwa uenyekiti, Mheshimiwa Museveni aliahidi kuwa chini ya uenyekiti wake atatoa ushirikiano wa kutosha kwa umoja huo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Nchi na Serikali wakati aliposhiriki ufunguzi wa mkutano wa 19 wa Wakuu wa Nchi na Serikali Zisizofungamana na Upande Wowote (NAM), katika ukumbi wa Ruwenzori, Kampala nchini Uganda, Januari 19, 2024. Waziri Mkuu amemuwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mkutano huo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Chapisha Maoni

0 Maoni