Ujenzi wa Kituo cha Utangazaji Utalii Kusini kuanza

 

Wizara ya Maliasili na Utalii kwa niaba ya Bodi ya Utalii Tanzania imesaini mkataba na kampuni ya Ujenzi ya Azhar Construction Ltd ya jijini Dar es Salaam wa ajili ya kujenga kituo cha utangazaji Utalii Kusini mwa Tanzania.

Ujenzi huo unatarajiwa kufanyika katika eneo la Kihesa Kilolo mkoani Iringa. Kituo hicho kitakachosimamiwa  na Bodi ya Utalii Tanzania ni utekelezaji wa Mradi wa uendelezaji wa Utalii Kusini mwa Tanzania (REGROW).               

Kituo cha Utangazaji Utalii kusini mwa Tanzania (ONE STOP CENTER) kitakuwa  na ghorofa sita ikiwa na kumbi za mikutano, migahawa, maduka ya bidhaa za kitalii, ofisi za Bodi ya Utalii na zile za wadau wa utalii. Ujenzi unatarajia kukamilika ndani ya miezi 12.

Matarajio ya sekta ya utalii, baada ya kukamilika kwa jengo hilo ni kuufungua utalii kusini mwa Tanzania, kuongeza mapato yatokanayo na sekta ya utalii, kuongeza idadi ya watalii na kuongeza idadi ya siku ambazo watalii wanakaa nchini. #tanzaniaunforgettable.



Chapisha Maoni

0 Maoni