Rais Samia ashiriki upandaji miti 27 YA KIJANI

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameungana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman pamoja na viongozi wengine katika zoezi la upandaji miti, Zanzibar.

Rais Samia na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Othman, wameshiriki zoezi hilo leo Jumamosi Januari 27 2024, wakiungana na viongozi wengine wa kitaifa pamoja wananchi mbalimbali, katika zoezi hilo la upandaji miti, huko Donge Muwanda, Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Zoezi hilo ambalo ni sehemu ya mpango wa kupambana na mabadiliko ya Tabianchi, limekwenda sambamba na kumbukizi ya siku ya kuzaliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Viongozi wengine ambao wamejumuika katika zoezi hilo lililobeba Jina la '27 YA KIJANI' ni pamoja na Mawaziri wa Serikali zote Mbili; Viongozi wa Jamii, Dini na Siasa, Watendaji mbali mbali, Wanamazingira, kutoka Ndani na Nje ya Nchi; na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, wote wakiongozwa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Mhandisi Zena Ahmed Said.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman, akipanda mti katika zoezi la upandaji miti la 27 YA KIJANI huko Donge Muwanda, Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman, katika zoezi la upandaji miti la 27 YA KIJANI huko Donge Muwanda, Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman, wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa kitaifa walioshiriki zoezi la upandaji miti la 27 YA KIJANI huko Donge Muwanda, Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Chapisha Maoni

0 Maoni