Mhe. Simai ajiuzulu Uwaziri wa Utalii Zanzibar

 

Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Simai Mohamed Said ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo jana usiku. 

Simai ambaye pia ni mwakilishi wa jimbo la Tunguu kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ametangaza kujiuzulu akisema ni kutokana na kile alichokiita ‘mazingira yasiyo rafiki ya kazi’.

Kupitia video fupi aliyojirekodi, Simai amesema kwamba tayari amemuandikia barua ya kujiuzulu Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi.

Chapisha Maoni

0 Maoni