Meli ya watalii yenye urefu wa mita 294 yatia nanga Dar

 

Meli ya watalii kutoka nchini Norway yenye urefu wa mita 294 imetia nanga katika Bandari ya Dar es Salaam ikiwa na watalii 2,210.

Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Mrisho Mrisho amesema ujio wa meli hiyo yenye uwezo wa kubeba abiria 4,700 kutafungua milango kwa wadau wengine wenye meli kubwa zaidi duniani kutia nanga kwenye bandari hiyo.

Chapisha Maoni

0 Maoni