Kenya na Tanzania wamaliza tofauti zao za usafiri wa anga

 

Serikali ya Kenya imeridhia kutoa kibali cha ndege ya mizigo ya Shirika la Ndege la Tanzania kutoa huduma ya usafirishaji mizigo kwa njia ya anga ya Kenya, kama ilivyombwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kufuatia hatua hiyo Serikali ya Tanzania nayo, imeondoa zuio la safari za ndege za Shirika la Ndege la Kenya (KQ), lililotolewa jana Januari 15, 2024 na ambalo lilipaswa kuanza utekelezaji wake Januari 22, 2024.

Taarifa iliyotolewa leo Januari 16, 2024 na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Anga Tanzania (TCAA) Hamza Johari, imeeleza kufikiwa kwa uamuzi huo wa kurejesha safari za KQ za Nairobi na Dar es Salaam.

Chapisha Maoni

0 Maoni