Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Moses Nnauye ameipongeza Kamapuni ya Huwawei kwa kuwezesha programu ya “Seed for the Future” inayochochea Vijana wa Kitanzania kushiriki kikamilifu katika Teknolojia za Kidijitali ambao wamehitimu mafunzo maalumu kuhusu program hiyo.
Mhe. Nape ametoa pongezi hizo wakati akizungumza katika
hafla ya kuwakabidhi vyeti vya kukamilisha mafunzo maalumu iliyoshirikisha
Vijana 14. Hafla hiyo imefanyika katika Hoteli ya Rotana Jijini Dar es Salaam.
Kampuni ya Huawei ilizindua programu yake ya kimataifa
inayowawezesha vijana kushiriki katika mafunzo ya teknolojia ya kidijitali.
Waziri Nape Nnauye aliipongeza Huawei kwa juhudi zao na
kuonyesha mipango na matumaini kuhusu athari chanya zinazotokana na programu
hiyo kwa vijana wa Tanzania.
Waziri Nape Nnauye alisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati
ya Serikali, makampuni binafsi, na Taasisi za Elimu ya Juu katika kuendeleza
ujuzi wa kidijitali miongoni mwa vijana.
Alizungumza katika hafla hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya
Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,
Bwana Mohammed Khamis Abdullah pia amewapongeza Huawei kwa kutoa fursa
kwa vijana wa Tanzania kwa kuwawezesha katika ubunifu wa kimataifa na kuwezesha
nia ya Serikali ya kukuza ujasiriamali kupitia
ubunifu kapitia TEHAMA.
0 Maoni