Watu wawili wafa kwa kula uyoga wenye sumu

 

Watu wawili ambao ni Mauwa Mwilikwa mwenye umri wa miaka 10 na Thomas Thomas mwenye miaka 18 wote wakazi wa Mabatini wamefariki dunia baada ya kusadikiwa kula uyoga wenye sumu.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Wilbroad Mutafungwa amesema tukio hilo limetokea tarehe 17 ya mwezi huu ambapo watu hao na wengine saba wanadaiwa kula mboga aina ya uyoga na kupelekea kutapika na kuharisha mfululizo hadi walipokimbizwa hospitali, ambapo Mauwa Mwilikwa alipelekwa hopsitali ya Rufaa ya kanda Bugando na Thomas Thomas alipelekwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza Sekou Toure ambapo wote wawili walifariki dunia.


Kamanda Mutafungwa ameongeza kuwa watu wengine saba bado wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa ya kanda Bugando kufuatia kula chakula hicho kinachosadkiwa kuwa na sumu.

Aidha, jeshi la polisi linaendelea kumsaka mtu aliyewauzia watu hao uyoga uliowasababishia madhara huku wengine wakipoteza maisha ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake.

Chapisha Maoni

0 Maoni