Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu
Hassan, ametoa msamaha kwa wafungwa 2,244 katika kuadhimisha miaka 62 ya Uhuru
wa Tanzania bara hii leo.
Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
imesema kati ya wafungwa hao wafungwa 263 wataachiwa huru leo, wafungwa 2
waliohukumiwa adhabu ya kifo wamebadilishiwa adhabu hiyo na kuwa kifungo cha
maisha.
Pamoja na mambo mengine taarifa hiyo ya Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi imesema pia wafungwa 1,979 wamepunguziwa sehemu ya adhabu zao
ambazo wataendelea kuzitumikia gerezani.
0 Maoni