Mkuu wa
Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Jacob John Mkunda kwa niaba
ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt Samia Suluhu
Hassan amewavisha nishani mbalimbali Majenerali, Maafisa na Askari wa JWTZ
jijini Tanga tarehe 04 Desemba 2024.
Nishani hizo
ni pamoja na Nishani ya Kumbukumbu ya Muungano Daraja la Nne, Nishani ya Utumishi Uliotukuka, Nishani ya Utumishi
Mrefu, Nishani ya Utumishi Mrefu na Tabia Njema, na Nishani ya Miaka 60 ya
JWTZ.
Aidha,
Jenerali Mkunda amewavisha nishani ya Jumuiya ya SADC Maafisa na Askari
walioshiriki Ulinzi wa Amani nchini Msumbiji chini ya mwavuli wa Jumuiya hiyo.
Jenerali
Mkunda amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu
Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan na Serikali kwa ujumla kwa kufanikisha Wanajeshi
kutunukiwa Nishani na pia amewapongeza Maafisa na Askari wa Kanda ya Tanga kwa
kutunikiwa Nishani hizo.
Amewataka
kuendelea kulinda Mipaka ya Nchi na Kufanya Mafunzo na Mazoezi ya hali ya juu
pamoja na kuyaishi Mambo Manne kwa Mwanajeshi ambayo ni Nidhamu, Uaminifu,
Uhodari, na Utii ili waweze kutimiza Majukumu
ya Ulinzi wa Nchi kwa ujumla.
0 Maoni