Hospitali ya
Taifa Muhimbili-Mloganzila imemkamata Bw. Kija Mayunga mkazi wa Dodoma
anayedaiwa kuwatapeli ndugu wa wagonjwa kwa madai ya kuwasaidia ili wapate
huduma.
Bw. Mayunga
tayari amefikishwa Kituo cha Polisi Gogoni kwa hatua zaidi.
Kufuatia
hali hiyo uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila unatoa wito kwa
wananchi kufuata utaratibu wa kupata huduma ikiwemo kufuata utaratibu wa malipo
uliowekwa na hospitali ili kuepuka matapeli.
0 Maoni