Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani
Kikwete amesema Serikali imejidhatiti kuweka mazingira yanayowezesha vijana
kutoka kwenye uchumi usio rasmi kuelekea uchumi ulio rasmi.
“Serikali
inaendelea kuimarisha sera zinazowezesha nguvu kazi ya taifa, kuondoa vikwazo
vya Kibiurokrasi, kutoa msaada wa kiufundi na kifedha kwa vijana,” amesema Mhe.
Ridhiwani.
Mhe.
Ridhiwani amebainisha hayo Jijini Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa uchambuzi
wa kina wa sekta isiyo rasmi katika biashara zinazoongozwa na vijana.
Aidha,
amesema tafiti zilizofanywa sekta zisizo rasmi zitasaidia kupata majawabu ya
matatizo ya Vijana katika kukabiliana na changamoto isiyo rasmi.
Uzinduzi huo
umehudhuriwa na Mkurugenzi wa Shirikia la Kazi Duniani Kanda ya Afrika
Mashariki Bi. Caroline Mugalla, Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu wa
ATE Bi. Suzanne Ndomba na Watafiti Mashuhuri.
0 Maoni