Jeshi la Polisi limesema kwamba linafuatilia tukio la kutekwa Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Ngome ya Vijana, Abdul Nondo baada ya kupokea taarifa hiyo leo Desemba mosi 2024 na kufungua jalada.
Nondo
anadaiwa kutekwa leo alfajiri katika stendi ya Magufuli eneo la Mbezi Louis wakati
akiwasili kutokea mkoani Kigoma kwa usafiri wa basi la Saratoga lenye namba za
usajili T 221 DKB.
Nondo
alikuwa sehemu ya viongozi wa kitaifa wa chama hicho walioongoza kampeni za
uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwenye mikoa ya magharibi mwa Tanzania.
Taarifa
iliyotolewa leo na Msemaji wa Jeshi la Polisi DCP David Misime imepokea taarifa
ya kutekwa kwa mtu mmoja mwanaume katika stendi ya Magufuli Mbezi Louis Dar es
Salaam.
Taarifa hiyo
imesema mtu huyo ametekwa kwa nguvu majira ya saa 11:00 alfajiri na kuchukuliwa
na watu waliokuwa wakitumia gari lenye usajili namba T 249 CMV aina ya
Landcruise rangi nyeupe.


0 Maoni