Rais Samia atembelea maeneo yaliyoathirika na maporomoko Hanang, awapa pole

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wa eneo la Jorodom ambalo limeathirika na Mafuriko pamoja na maporomoko ya matope na mawe Wilayani Hanang Mkoani Manyara tarehe 7 Desemba, 2023. Rais Samia alijionea uharibifu mkubwa uliotokea na kuwapa pole Waathirika wa maafa hayo na kuwaeleza kuwa Serikali ipo pamoja nao.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Ndugu Elibariki Naman mkazi wa Jorodom, Katesh ambaye ni muathirika wa maporomoko ya matope na mawe yaliyotokea Wilayani Hanang. Ndugu Elibariki alikuwa akielezea jinsi majirani zake walivyopoteza maisha pamoja na makazi yao katika maafa hayo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga akielezea kuhusiana na athari za maporomoko ya matope na mawe yaliyotokea katika eneo la Jorodom Katesh Wilayani Hanang. Rais Samia ametembelea eneo hilo Mkoani Manyara tarehe 7 Desemba, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimfariji muathirika wa maporomoko yaliyotokea Katesh Bi. Salome Elifuraha ambaye amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Tumaini iliyopo Katesh, Hanang. Mama amepoteza watoto wawili kwenye maafa hayo huku mtoto wa tatu akiwa bado hajapatikana hadi sasa. Rais Samia aliwatembelea majeruhi wa maafa ya mafuriko hayo ambao wamelazwa katika hospitali hiyo ya Wilaya Mkoani Manyara tarehe 7 Desemba, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amembeba mtoto Wina Joseph mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi 8 ambaye pia yeye na mama yake ni waathirika wa maporomoko yaliyotokea Katesh Wilayani Hanang. Rais Samia aliwatembelea majeruhi wa maafa ya mafuriko hayo ambao wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Tumaini, Hanang Mkoani Manyara tarehe 7 Desemba, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa ndani ya Helikopta na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga wakati wakiangalia athari za maporomoko ya matope na mawe yaliyotokea katika mji mdogo wa Katesh pamoja na vijiji jirani, Hanang Mkoani Manyara tarehe 7 Desemba, 2023.

Chapisha Maoni

0 Maoni