WAJASIRIAMALI kutoka maeneo mbalimbali nchini Tanzania
wamemshukuru Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwawezesha kushiriki
maonesho ya 23 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki maarufu Nguvu Kazi au Jua Kali yanayofanyika Bujumbura, Burundi
kuanzia tarehe 5 hadi 15 Desemba, 2023.
Wakizungumza Wajasiriamali hao kwa nyakati tofauti wamesema
uratibu uliofanywa na Serikali kugharamia usafiri wao na mizigo, hali hiyo
imewapa chachu ya kushiri kwa wingi zaidi. Pia, wamepongeza juhudi nahatua
mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali chini ya uongozi Madhubuti wa Mheshimiwa
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa
kuendelea kuweka mazingira wezeshi ya biashara ikiwa ni pamoja na kuwawezesha
kushiriki maonesho hayo.
“Sisi wajasiriamali tunafarijika sana kuona serikali yetu
inatujali sana kwa kutupatia fursa hii muhimu ili tuweze kutangaza biashara
zetu katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki,” amesema Bi. Ester
Ngalawa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Ajira na Ukuzaji Ujuzi kutoka
Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Ally Msaki amesema Serikali imeendelea kuwezesha
Wajasiriamali Wadogo na wa Kati kutangaza biashara zao nje ya mipaka ya
Tanzania.
Sambamba na hayo amehamasisha wananchi wa Burundi
kutenmbelea mabanda ya wajasiriamali wa Tanzania ili kujionea bidhaa za ubunifu
zinazozalishwa na wajasiriamali hao.
Naye Afisa Biashara Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
(EAC), Monica Miyigo amesema maonesho hayo yamevutia Wajasriamali Zaidi ya
1,500 kutoka nchi zote saba (7) wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Maonesho hayo yanaongozwa na kauli mbiu “Kuunganisha Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Afrika Mashariki kufanya biashara katika eneo la Jumuiya ya Afrika Mashariki,”. Yanalenga kutoa fursa kwa wajasiriamali kuonesha huduma na bidhaa mbalimbali wanazozalisha, kubadilisha uzoefu, ujuzi na taarifa na wajasiriamali wenzao katika Jumuiya sambamba na kukuza wigo wa masoko mapya.
Na. Mwandishi Wetu- Burundi
0 Maoni