Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Geofrey Pinda amemaliza na kuufunga wa wananchi 767 wa Kiegeya mkoani Morogoro.
Wananchi hao ni wale waliovamia na kulima katika shamba la
Tungi Sisal Estate la Mwekezaji Star Infrastructure.
Mhe Pinda amemaliza na kuufunga mgogoro huo alipokutana na
wawakilishi wa wakulima wakioongozwa na Mwenyekiti wao Haleluya Minga katika
ofisi ya Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Morogoro.
Naibu Waziri wa Ardhi alifika mkoani Morogoro kwa ajili ya
kuwasikiliza ili kupata ukweli ambapo baada ya kuwasikiliza kwa takriban saa
nne alibaini udanganyifu katika maelezo ya wakulima na kuwapa taarifa kuwa
mwekezaji ni mmiliki halali na alitoa ekari 4000 alizoombwa na serikali na wao
wamevamia sehemu mpya.
‘’Niwatake muwe waungwana na mfuate taratibu za kisheria za
kupata ardhi na hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa wale wakataokaidi
maelekezo ya serikali na mgogogoro huu kuhusu wananchi 767 nimeufunga rasmi’’
alisema Pinda.
‘’Kesi yenu ilipitiwa
katika ngazi mbalimbali na utafiti wake umefanyika mpaka uwandani na kuonesha
kuwa ninyi hamna haki, kwanza mko tofauti na idadi yenu inaongezeka kila siku
kutoka 319 hadi 767 na bado inaendelea hivyo katika mazingira ya kawaida
inawawia vigumu kuwasaidia’’ alisema Mhe. Pinda.
Mwenyekiti wa wakulima hao Haleluya Minga mbali na
kumshukuru Naibu Waziri kwa kuamuzi wake wa kwenda kuwasikiliza wakulima hao
alimueleza kuwa, kuongezeka kwa idadi ya wakulima kulitokana na wao kutokuwa na
utaratibu wa vikao na baada ya kugundua hilo ndipo walipokutana na kuchagua
uongozi.
‘’Kupanda kwa idadi ya wakulima kutoka 319 hadi 767, kwanza
hatukuwa na utaratibu wa viakao na tulikuwa hatufahamiani na ilifika mahali
kulikuwa na ongezeko tukaamua kuwa na uongozi wa pamoja’’ alisema Haleluya.
Hata hivyo, Naibu Waziri Pinda amewataka wakulima hao kuwa
watulivu na matumizi ya nguvu hayatasaidai kwa kuwa kamati ya mkoa, ofisi ya
mkurugenzi wa manispoaa ya Morogoro na ile ya Taifa zinethibitisha kuwa wao
siyo wamiliki halali wa maeneo hayo.
Awali Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Morogoro Frank
Minzikunte alieleza historia ya shamba hilo kuwa inaanzia mwaka 1951 kwa
kumilikishwa kwa Mwekezaji na mwaka 1983 serikali ilimuomba mwekezaji ekari
4000 kwa muda ili wananchi wafanye kilimo cha kufa na kupona.
Aliongeza kuwa, mwaka 2021 serikali ilimuomba mwekezaji
kuziachia moja kwa moja ekari hizo ambapo baada ya majadiliano ya muda mrefu
mwekezaji aliridhia na wananchi waliokuwa wamepewa mwaka 1983 wakatambuliwa na
takriban wananchi 3777 walitambuliwa na kuingia mkataba na halmashauri ya
upimaji shirikishi kama ilivyoelekezwa na serikali.
Hata hivyo, Kamishna huyo wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Morogoro
alisema, wakati kutambua wananchi hao lilijotokeza kundi la wananchi 319 waliodaia
kulima nje ya ekari zilizotolewa na mwekezaji kwa wakulima na ndipo serikali
kupitia Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Na Munir Shemweta- WANMM Morogoro
0 Maoni