Miili miwili yashindwa kutambulika Hanang

Mwili mmoja zaidi umepatikana na kufanya miili ya watu waliokufa kwenye maporomoko ya matope, mawe na magogo wilayani Hanang mkoani Manyara kufikia watu 89.

Taarifa iliyotolewa leo na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Mobhare Matinyi imesema hadi sasa miili iliyopatikana ni 89 na miili 87 imeshatambuliwa na kuchukuliwa na ndugu zao kwa ajili ya mazishi. 

Akitoa taarifa hiyo ya Serikali ya maendeleo na hali baada ya kutokea maafa hayo Bw. Matinyi ameongeza kwa kusema kuwa kutokana na kuharibika vibaya, miili miwili bado haijatambuliwa.

Bw. Matinyi ambaye amepiga kambi huko Katesh tangu yatokee maafa hayo amesema jumla ya majeruhi waliopokelewa tangu maafa yatokee ni 139 lakini waliopo hospitalini ni 17.

Majeruhi 120 waliolazwa wamesharuhusiwa kutoka hospitali, isipokuwa watu wawili ambao walifariki dunia walipokuwa wanapatiwa matibabu, amesema Matinyi.

Chapisha Maoni

0 Maoni