MCC kuipatia tena Tanzania msaada wa dola za Marekani

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Changamoto za Millenia (MCC) Bi. Alice Albright kwa njia ya video, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma jana. 

MCC imeichagua tena Tanzania kuingia katika mpango wa kupata msaada wa fedha zitakazolenga kusaidia mabadiliko ya Sera na Kitaasisi nchini ili iweze kufanikiwa kupata mpango wa Compact. 

Mara ya mwisho Shirika la Changamoto za Millenia (MCC) lilikutoa msaada wa Fedha wa Dola za Kimarekani milioni 698 mwaka 2008 ambazo zilitumika hadi 2013.

Chapisha Maoni

0 Maoni