Likizo Time kunongesha msimu wa Sikukuu kwa watu 50

Bodi ya Utalii Nchini (TTB) kwa kushirikiana na Tanzania House of Talent wamezindua kampeni ya “Likizo Time” ambapo watatoa nafasi zaidi ya 50 kwa watanzania ili kusherehekea Msimu huu wa sikukuu kwenye Hoteli kubwa za Kitalii, pamoja na kutembelea vivutio vya Utalii vilivyopo maeneo mbalimbali ya nchi, Lengo la kampeni hii ni kuhamasisha Watanzania kufanya utalii wa ndani.                                                                      

Kampeni hii itakuwa endelevu kwenye sikukuu mbalimbali na itakuwa na punguzo la hadi asilimia 50% ili kuweza kujishindia nafasi hii adhimu tembelea mitandao ya kijamii ya tanzania_unforgettable.                                                                                                                   

Kampeni hiyo imezinduliwa leo na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania Bw Damas Mfugale katika Hoteli ya Johari Rotana jijini Dar es Salaam wakati wa kikao cha uhamasishaji wa Likizo Time na waandishi wa Habari.

Chapisha Maoni

0 Maoni